Katika
ulimwengu wa vyakula, inafahamika na kuaminika kuwa chakula ni dawa.
Chakula unachokula leo ndicho kinachoamua hali yako ya kiafya kesho.
Unaweza kuishi bila kuugua kama ukila vyakula vyote muhimu
vinavyohitajika mwilini.
Leo
nitakutajia orodha ya juisi zilizotengenezwa kwa matunda na mboga na
fadia zake mwilini. Katika orodha hii, utaona kuna mchanganyiko wa
matunda au mboga mbili hadi nne na kazi zake mwilini, zikitumika kama
tiba au kinga ya magonjwa.
KAROTI, TANGAWIZI NA TUFAHA(APPLE)
Juisi yenye
mchanganyiko wa matunda hayo matatu huondoa sumu mwilini na kuimarisha
mfumo wa kinga ya mwili. Tufaha ndiyo apple kwa Kiingereza.
TUFAHA, TANGO NA FIGILI
Juisi yenye
mchanganyiko wa matunda haya ni kinga dhidi ya saratani, huondoa lehemu
(cholestrol) mwilini, husafisha tumbo na pia huondoa maumivu ya kichwa.
NYANYA, KAROTI NA TUFAHA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya ngozi ya mwili mzima kuwa nyororo na huondoa harufu mbaya mdomoni.
TANGO CHUNGU,
TUFAHA NA TANGO LA KAWAIDA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huondoa harufu mbaya mdomoni na hupunguza joto la mwili.
CHUNGWA, TANGAWIZI NA TANGO
Juisi yenye
mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi na kuifanya kuwa
laini. Pia hupunguza joto la mwili. Kwa wale wenye matatizo ya kuwa na
ngozi kavu, juisi hii itawasaidia sana.
NANASI, TUFAHA NA TIKITIMAJI
Juisi yenye
mchanganyiko wa matunda haya hufanya kazi ya kuondoa chumvi nyingi
mwilini, husafisha kibofu cha mkojo na figo. Juisi hii ni nzuri kwa wale
wenye matatizo ya kibofu na figo au wanaotaka kujikinga na magonjwa
hayo.
TUFAHA, TANGO NA ‘KIWI’
Juisi yenye
mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi. Kiwi ni aina ya
matunda ambayo hujulikana pia kama ‘matunda-damu’.
PEASI NA NDIZI
Juisi yenye
mchanganyiko wa matunda haya hurekebisha kiwango cha sukari katika damu.
Inawafaa sana wagonjwa wa kisukari na inaweza kuwa sawa na kinga dhidi
ya ugonjwa huo.
KAROTI, PEASI, TUFAHA NA EMBE
Juisi yenye
mchanganyiko wa matunda haya huzuia athari ya sumu mwilini, hupunguza
shinikizo la damu na kuondoa mlundikano wa uchafu mwilini.
MASEGA YA ASALI, ZABIBU, TIKITIMAJI NA MAZIWA
Juisi yenye
mchanganyiko huu huwa na kiasi kikubwa cha Vitamin C na Vitamin B2
ambazo huimarisha chembechembe hai na kinga ya mwili.
Juisi hii
ina kiwango kikubwa cha Vitamin C, E na madini chuma. Huimarisha rangi
ya ngozi na mfumo wa usagaji wa chakula tumboni.
Juisi hii yenye kiasi kikubwa cha vitamini na virutubisho mbalimbali vyenye faida mwilini, huzuia tatizo la ukosefu wa choo.
Ili kupata
faida hizo zilizoainishwa katika kundi la matunda hayo, usafi wa matunda
yenyewe hauna budi kuzingatiwa wakati wa kutayarisha juisi yake.
Vilevile hakikisha unatumia matunda yaliyoiva vizuri na uyatayarishe kwa
kuzingatia kanuni ya ‘mtu ni afya’.
Unaweza
kutumia mashine maalumu ya kukamulia matunda (blender) au kutumia njia
ya asili ya kutwanga kwa kinu maalumu na kupata juisi hiyo. Kama
utaongeza sukari, inashauriwa kuweka kiasi kidogo sana. Ni bora zaidi
usipoweka sukari, kwa sababu matunda mengi yana sukari ya asili.
No comments:
Post a Comment